I am a CHAMPION!

I will conquer what has not been conquered, defeat will not be in my creed,

I will believe what others have doubted,

I will always endeavor the prestige, honor, and respect of my team,

I have trained my mind and my body will follow,

Who am I?

I am a CHAMPION!

Facebook

Thursday, October 6, 2011

Lesson from Steve Jobs of Apple!

“Your time is limited, so don’t waste it living someone else’s life. Don’t be trapped by dogma – which is living with the results of other people’s thinking. Don’t let the noise of other’s opinions drown out your own inner voice. And most important, have the courage to follow your heart and intuition. They somehow already know what you truly want to become. Everything else is secondary.” SJ


Yawezekana ulipofungua ama kuingia kwenye mtandao kufanya lolote lile uliilotaka kufanya leo hii ukakutana na taarifa za kifo cha Steve Jobs, na kama wewe ni mtumiaji wa kompyuta za Apple ama brauza ya safari utakuwa ulikutana na picha ya Bwana huyu ikieleza umri kuzaliwa na kufa kwake.
 

Inawezekana kabisa si wengi wanamfahamu au waliwai kusikia juu ya mtu huyu ambaye leo vyombo vyote vya habari (vya nje) na mitandao vinaanikiza juu ya kifo cha Mbunifu huyu mwenye kuheshimika duniani.

 Bila shaka kama ulikuwa humjui au hukumfahamu hapo kabla leo utakuwa umemfahamu  japo kidogo kupitia kifo chake, sina nia ya kukujuza juu ya msiba huu au umetokeaje na vitu kama hivyo, hapana, nia yangu ni kutaka tujifunze kwa pamoja sisi kama wajasiriamali juu ya mjasiliamali huyu asiyekata tama kirahisi. Jeni funzo gani tunapata kupitia historia ya maisha yake?

 Kama umepata muda kupitia historia yake utakuwa umegundua kuwa haina chochote cha kufanya na mafanikio yake, kwanza hakulelewa na wazazi wake, kwani baada ya kumzaa walimasili (adopted) kwa wazazi wengine, pili, ubunifu wake hauna uhusiano wowote na elimu yake, kwani aliweza kukaa chuo cha ufundi cha gharama wakati huo miezi sita tu ama muhula Mmoja, hakumaliza chuo, aliishi maisha ya kutangatanga na kuvutiwa zaidi na kazi za mafundi umeme wa magari ambayo ndio ilikuwa kazi ya baba yake (sio mzazi).
 
In this rare photograph, you can see how Steve Jobs looked at the lowest point of his career.
It was taken for Andy Hertzfeld’s birthday in April 1993.
From left to right: Mac programmer Andy Hertzfeld, Lisa and Mac programmer Bill Atkinson, Mac programmer and NeXT co-founder Bud Tribble, and Steve

Tunachokiona ni kuwa toka akiwa mdogo alivutiwa na kutamani kujua zaidi juu ya mambo ya vufaa vya umeme, hapa ndipo alipojenga ukaribu na jamaa Mmoja aliyekuwa akifanya kazi kiwanda cha kompyuta HP Wakati huo, Woz akajenga mazoea kwenda kujifunza nyumbani kwa Woz, akajiunga naye na hatimaye  akamua kununua sehemu ya mradi wa Woz wa Apple, akiwa na nia ya kutengeneza kompyuta bora kabisa duniani akiwa na umri wa miaka 20 tu, wawili hao wakiwa na kamtaji kadogo sana, lakini wakiwa ndoto kuuubwa ya kuubadili ulimwengu kiteknolojia walianza ubunifu kufikia ndoto zao. 
“Sometimes when you innovate, you make mistakes. It is best to admit them quickly, and get on with improving your other innovations.” SJ

Steve alianza kutengeza Apple nyumbani kwake na kuzitembeza madukani, waliweza kuuza japo kwa taabu kidogo kwani yao ilikuwa bodhaa mpya na soko limeshikiliwa na IBM, waliamua kuziongezea ubora kwa kuweka program zaidi na hatimaye baada ya muda walifanikiwa kukamata soko na hivyo miaka mine tangu kuanzishwa ikawa ni kampuni kubwa kiasi cha kuingia soko la hisa, mwaka wa tano walitengeneza faida kubwa kufikia Dola million 200, hivyo kuwa Millionea akiwa na miaka 25 tu.


 Haya yalikuwa mafanikio makubwa sana kwa Steve, lakini pia yalikuja yakiwa yameambatana na majaribu yake, kwani kampuni ilianza kufanya vibaya kiasi cha kufikia kufukuzwa katika kampuni aliyoianzisha na kuamua kuuza hisa zake zote na kuendelea na maisha yake, lakini hakuuza maono wala ndoto zake.
 “I’m convinced that about half of what separates the successful entrepreneurs from the non-successful ones is pure perseverance.” SJ
 Hii ilikuwa ni mwaka 1985, steve aliamua kuendeleza ubunifu wake kwa kuanzisha kampuni mbali mbali za kutengezea programu mbali mbali za kompyuta, hata hivyo hazikuweza kufanya vizuri katika soko, miaka takrina tisa ilikuwa migumu kwake, ilifika mahali akakaribia kukata tamaa, hii ilikuwa mwaka 1993, kwa maneno yake anasema “ankle dip shit”.


 Huko msemo usemao “It is always dark before dawn” au ukiona kiza kimezidi kumekaribia kucha, pengine ndio unaoweza elezea mazingira ya kuibuka tena upya  kwa Steve na hatimaye kufikia mafanikio aliyoyoacha nyuma yake.

 Mwishoni mwa mwaka 1993 akiwa bado ana maono yake na ndoto zake zikiwa hazijaathiriwa na mawimbi ya mkwamo wa kibiashara alianza upya kuboresha bidhaa zake na hivyo kujaribu kuziuza upya kwa makampuni na vyuo, aliamua pia kutengeneza programu ya mwanasesere, alijaribu kutaka kuiingiza katika soko la hisa, akawaona wataalamu wa masoko na wachambuzi, walimcheka sana, walimwona kama anayeota ndoto ya mchana, kampuni yake ilikuwa ikifanya vibaya kwa kipindi cha miaka tisa mfululizo.
“I didn’t see it then, but it turned out that getting fired from Apple was the best thing that could have ever happened to me. The heaviness of being successful was replaced by the lightness of being a beginner again, less sure about everything. It freed me to enter one of the most creative periods of my life.” SJ

 Hakukata tamaa, alikuwa na maono ya mbali na zaidi aliamini kuwa INAWEZEKANA, kutokana na kutokata tama kwake kwa jambo analoamini kuwa linawezekana, miaka miwili baadaye 1995 alipata mafanikio makubwa kupitia programu yake iliyokataliwa kwanza na wataaalumu na hivyo kumuingizia Dola Billioni 1.5, ikiwa ni mara tano zaidi ya alizowai kuingiza akiwa na Apple, huo ulikuwa mwanzo wa mafanikio na hatimaye kurudi tena Apple Macntoshi na kuendeleza ndoto yake ya kubadili ulimwengu kupitia teknologia. 
 “You know, I’ve got a plan that could rescue Apple. I can’t say any more than that it’s the perfect product and the perfect strategy for Apple. But nobody there will listen to me.” SJ



Kutokana historia yake nimejifunza mambo mengi sana, hapa chini ni machache tu:-

  • Kufanikiwa katika jambo lolote maishani  hakuna uhusiano na historia yako au hali ya uchumi ya wazazi wako.
  • Kufanikiwa kwako hakuna uhusiano wa moja kwa moja na elimu yako au wazazi wako. 
  • Kufanikiwa hakuna uhusiano na kazi unayofanya bali fikira na ndoto ulizonazo.
  •  Kufukuzwa kazi si mwisho bali ni mwanzo wa kunoa akili na kutumia ubunifu wako kufikia ndoto zako. 
  • Kushindwa (Failure) ni mwalimu mzuri sana maishani. 
  • Kutokutaka tamaa, kung'ang'ania kile unachokiamini pasipo kujali wengine wanasema nini juu yake ndio msingi mkuu wa kutimiza ndoto zako. NK.  

Winners Boulevard 0784 475576, 0716927070.  For comment or ideas

No comments:

Subscribe via email

Pata nakala ya mada hizi moja kwa moja katika email yako hapa.

Delivered by FeedBurner

SUCCESS

If these qualities describe you...

1. Self Motivated

2. Highly Ambitious

3. Big Thinker

4. Entrepreneurial

5. Not Willing to Settle for Less

6. Goal Oriented

7. Want to Be Your Own Boss,

8. Want to Live a Life by Design

9. Confident in Making Decisions

10. 200% Committed to change your life within the Next 6-12 Months. You read that right - 200%!!

...then, subscribe to the email ABOVE to contact us ASAP to get:-

• A success—and achievement—oriented articles

• Success quotes to motivate and inspire you

• Special offers on new and best-selling personal achievement resources

• Occasional articles from World renown top experts in personal achievement.